KAGAME ATANGAZA MAOMBOLEZO SIKU TATU

Rais Paul Kagame wa Rwanda, ametangaza siku tatu za maombolezo kuanzia kesho Jumatatu kuomboleza kifo cha Rais Mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu wa Rwanda, wakati wa siku tatu za maombolezo bendera ya taifa ya nchi hiyo na ile ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti.

Mkapa alifariki dunia hospitalini Dar es Salaam Alhamisi usiku, Julai 23.

Mwishoni mwa wiki Rais Kagame aliagiza nchi hiyo iungane na wananchi wa Tanzania kuomboleza kifo cha Mkapa hadi keshokutwa ambapo pia ni siku ya maziko ya kiongozi huyo.

@ikulu_mawasiliano @ikulu_habari
#dailynewsdigitalupdate #habarileoupdate #spotileo#ccm #ripmkapa

Post a Comment

0 Comments