KAULI YA FAMILIA KUHUSU SABABU ZA KIFO MZEE MKAPA

FAMILIA  YATOA KAULI KUHUSU KIFO CHA BABA YAO

Hayo yameelezwa katika Shughuli za kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Rais Wsataaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Benjmini William Mkapa zilizoanza rasmi leo katika Uwanja Uhuru jijini Dar es salaam mapema leo asubuhi.

 Shughuli za kuaga mwili  zimetanguliwa na ibada ya misa takatifu iliyoongozwa na Mwashamu Aakofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Iringa na kwa kushirikiana na Maaskofu kutoka Jimbo la Tanga na Jimbo la Njombe.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. DKT. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi na watumishi mbalimbali wa serikali,viongozi wa dini, na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati wa kutoa neno Msemaji wa familia ya Mzee Mkapa ameishukuru serikali, viongozi wa dini na wananchi wote kwa jinsi wanvyowakimbilia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Pia ametumia nafasi hiyo kueleza sababu ya kifo cha Hayati Mzee Mkapa na kuwataka waombolezaji kuupuuza taarifa za uzushi zinazoenezwa na baadhi ya watu wasiokuwa na nia njema na familia na hata taifa kwa ujumla. 

Aidha msemji huyo wa familia amewataka Watanzania kuamini taarifa zilitolewa na familia ndio taarifa halali na sahihihi kuhusu kifo cha Mzee Mkapa na sio vinginevyo.ameeleza sababu ya kifo ni mshutuko wa moyo

Post a Comment

0 Comments