Aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi aelezea umakini wa Mkapa katika kuandaa hotuba zake
Katibu Kiongozi Mstaafu Ombeni Sefue alielezea uzoefu wake kipindi alipokuwa Msaidizi na Mwandishi wa Hotuba wa marehemu Rais Mstaafu Benjamin Mkapa kwa kipindi chake chote cha uongozi miaka 10.
Alisema wakati alipokuwa anaandika hotuba za rais huyo alijifunza mengi hasa kujua hisia za kiongozi huyo, anataka nini na ni ujumbe gani anataka kuufikisha kwa wananchi wake.
“Nilikuwa naandaa rasimu za hotuba yake anazisoma kwa makini na kuzipitisha kwa kweli ukiandaa hotuba ya rais lazima uelewe anataka nini na lazima uwe makini kwa sababu, Mkapa alikuwa mtu makini sana hivyo rasimu yako lazima uifanyie kazi ya kutosha,” alieleza Ombeni.
Alisema moja ya hotuba ambayo anaikumbuka kumgusa wakati akiandaa ya Mkapa ni ile aliyoisoma katika maziko ya hayati Mwalimu Julius Nyerere.
“Ile hotuba ilininyima usingizi kwa sababu nilikuwa natakiwa lazima nielewe hisia zake, ujumbe wake na anataka kusema nini kwa wananchi wake,” alisisitiza.
0 Comments